KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Yote Namtolea Yesu

 1. Yote namtolea Yesu,
  Nampa moyo wote,
  Nitampenda siku zote,
  Namwandama kila saa.

 2. Yote kwa Yesu,
  Yote kwa Yesu,
  Yote kwako, Ee Mwokozi,
  Natoa sasa.

 3. Yote namtolea Yesu,
  Nainamia pake;
  Nimeacha na anasa,
  Kwako Yesu nipokee,

 4. Yote namtolea Yesu,
  Nifanye niwe wako;
  Nipe Roho yako, Bwana,
  Anilinde daima,

 5. Yote namtolea Yesu,
  Nami naona sasa;
  Furaha ya ukombozi,
  Nasifu jina lake.


TenzizaRohoni

ADS