KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Yesu Nakupenda, U Mali Yangu
(My Jesus I Love Thee, I know Thou art mine)

 1. Yesu nakupenda, U mali yangu,
  Anasa za dhambi sitaki kwangu
  Na Mwokozi aliyeniokoa,
  Sasa nakupenda, kuzidi pia.

 2. Moyo umejaa mapenzi tele
  Kwa vile ulivyonipenda mbele,
  Uhai wako ukanitolea
  Sasa nakupenda, kuzidi pia.

 3. Ulipoangikwa Msalabani
  Tusamehe tulio dhambini
  Taji ya miiba uliyoivaa
  Sasa nakupenda, kuzidi pia.

 4. Niwapo hai, niwapo maiti
  Kupendana nawe kamwe siachi;
  Hari za kifo zikinienea,
  Sasa nakupenda, kuzidi pia.

 5. Mawanda mazuri na maskani
  Nivatazamapo huko mbinguni,
  Tasema na taji nitakayovaa
  Sasa nakupenda, kuzidi pia.


TenzizaRohoni

ADS