KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Wewe Umechoka Sana?
(Art thou weary, art thou languid?)

 1. Wewe umechoka sana?
  Wataka raha?
  Kwake Yesu utapata
  Furaha.

 2. Alama anazo Yeye?
  Sasa! makovu
  Ya mikono, na miguu,
  Na mbavu.

 3. Nacho kimevikwa taji
  Kichwa cha huba?
  Alivikwa taji kweli
  Miiba.

 4. Huku nikimtafuta
  Nipate nini?
  Maonjo nje na ndani
  Amani.

 5. Kwamba namwandama
  Bwana,
  Mwisho ni nini?
  Ni furaha na salama
  Mbinguni.


TenzizaRohoni

ADS