KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Waitwa, Mwovu, na Bwana
(Beulah Land)

 1. Waitwa, mwovu, na Bwana
  Umwendee hima sana,
  Usafiwe dhambi zako,
  Humwoni ni mwema wako?

 2. Unaitwa! Itika tu!
  Umwendee Bwana Yesu!
  Sifiche makosa yako,
  Uungame dhambi zako!
  Kristo tu umuamini,
  Ndiyo njia ya Mbinguni.

 3. Alilipa damu yake
  Ili kukukweza kwake
  Alikufa yeye Bwana
  Mimi nawe tuwe wema.

 4. Ukifanywa kuwa mwema
  Mwishoni utasimama,
  Utaingia rahani
  Na wapenzi wa zamani.

 5. Ni mwanga tu, nchi lie,
  Uovu hauko kule,
  Kwamba wataka ufike
  Sharti huku uosheke.


TenzizaRohoni

ADS