KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Waimba, Sikizeni

 1. Waimba, sikizeni,
  Malaika mbinguni;
  Wimbo wa tamu sana
  Wa pendo zake Bwana;
  "Duniani salama,
  Kwa wakosa rehema."
  Sisi sote na twimbe
  Nao wale wajumbe;
  Waimba, sikizeni,
  Malaika mbinguni.

 2. Ndiye Bwana wa mbingu,
  Tangu milele Mungu,
  Amezaliwa mwili,
  Mwana wa mwanamwali;
  Ametoka enzini
  Kuja ulimwenguni
  Mwokozi atufie,
  Ili tusipotee,
  Waimba, sikizeni,
  Malaika mbinguni.

 3. Seyidi wa amani
  Ametoka Mbinguni,
  Jua la haki, ndite
  Atumulikiaye;
  Amejivua enzi,
  Alivyo na mapenzi,
  Ataka kutuponya,
  Kutuzalisha upya,
  Waimba, sikizeni,
  Malaika mbinguni.

 4. Njoo upesi, Bwana,
  Twakutamani sana;
  Kaa nasi, Mwokosi,
  Vita hatuviwezi;
  Vunja kichwa cha nyoka,
  Sura zako andika,
  Tufanane na Wewe,
  Kwetu sifa upewe,
  Waimba, sikizeni,
  Malaika mbinguni.


TenzizaRohoni

ADS