KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Twende kwa Yesu
(Come to the Saviour, make no delay)

 1. Twende kwa Yesu mimi nawe,
  Njia atwonya tuijue
  Imo Chuoni; na Mwenyewe,
  Hapa asema, Njoo!

 2. Na furaha tutaiona,
  Mioyo ikitakata sana,
  Kwako, Mwokozi, kuonona,
  Na milele kukaa.

 3. "Wana na waje," atwambia.
  Furahini mkisikia;
  Ndiye mfalme wetu pia,
  Na tumtii, Njoo.

 4. Wangojeani? Leo yupo;
  Sikiza sana asemapo;
  Huruma zake zikwitapo,
  Ewe kijana, Njoo.


TenzizaRohoni

ADS