KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Twamsifu Mungu

 1. Twamsifu Mungu kwa Mwana wa pendo,
  Aliyetufia na kupaa juu.

 2. Aleluya! Usifiwe, Aleluya! Amin.
  Aleluya! Usifiwe. utubariki.

 3. Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
  Ametufunulia Mwokozi wetu.

 4. Twamsifu Mwana, aliyetufia,
  Aliyetwaa dhambi akazifuta.

 5. Twamsifu Mungu wa neema yote,
  Ametukornboa akatuongoza.

 6. Tuamshe tena, tujaze na pendo,
  Na moyoni uwashe moto wa Roho.


TenzizaRohoni

ADS