KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Tafuta Daima Utakatifu

 1. Tafuta daima utakatifu;
  Fanya urafiki na Wakristo tu:
  Nena siku zote na Bwana wako;
  Baraka uombe kwa kila jambo.

 2. Tafuta daima utakatifu;
  Uwe peke yako ukimwabudu;
  Ukimwangalia Mwokozi wako,
  Utabadilishwa kama alivyo.

 3. Tafuta daima utakatifu;
  Kiongozi wake awe Yesu tu;
  Katika furaha au huzuni
  Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

 4. Tafuta daima utakatifu;
  Umtawaze Roho moyoni mwako;
  Akikuongoza katika haki,
  Hufanywa tayari kwa kazi yake.


TenzizaRohoni

ADS