KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Peleleza Ndani Yangu

 1. Peleleza ndani yangu,
  Iwe safi nia,
  Kwangu kama kwako Mungu,
  Idhihiri pia.

 2. Peleleza moyo wangu,
  Unifunulie,
  Yaliyomo ndani yangu,
  Nami niyajue.

 3. Kwanza washe zako tambi,
  Kumefunga giza;
  Nijue ambavyo dhambi,
  Ni la kuchukiza.

 4. Peleleza na mawazo,
  Ni mbegu za mambo,
  Asili ya machukizo,
  Maumbuo - umbo.

 5. Zidi kuyapeleleza,
  Katikati yangu,
  Hata wishe nifundisha
  Udhaifu wangu.

 6. Hapo nikikwinamia,
  Mbele zako, Mungu,
  Hakika nitakujua,
  U mpenzi wangu.


TenzizaRohoni

ADS