KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Panda Asubuhi Mbegu ya Fadhili

 1. Panda asubuhi, Mbegu ya fadhili,
  Panda adhuhuri tena jioni;
  Tutaingojea siku ya mavuno,
  Tutafurahi kuleta mavuno.

 2. Leta mavuno, Leta mavuno,
  Tutafurahi kuleta mavuno,
  Leta mavuno, Leta mavuno,
  Tutafurahi kuleta mavuno.

 3. Na panda mwangani, Tena kivulini
  Usiwe na hofu kwa baridi kuu;
  Na mwisho wa kazi kuvuna mavuno,
  Tutafurahi kuleta mavuno.

 4. Mvunieni Bwana, Kwa machozi mengi,
  Ijapo twaona taabu nyingi;
  Mwisho wa kilio tutakaribishwa,
  Tutafurahi kuleta mavuno.


TenzizaRohoni

ADS