KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Njoni Na Furaha, Enyi Wa Imani

 1. Njoni na furaha, enyi wa imani,
  Njoni Bethilehemu upesi!
  Amezaliwa jumbe wa Mbinguni,
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.

 2. Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga,
  Amekuwa radhi kuzaliwa,
  Mungu wa kweli, wala si kiumbe,
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.

 3. Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu,
  Mbingu zote na zijae sifa,
  Sifuni Mungu aliye Mbinguni,
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.

 4. Ewe Bwana mwema, twakubarikia,
  Yesu, utukufu uwe wako,
  Neno la Baba limekuwa mwili,
  Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
  Njoni tumuabudu Mwokozi.


TenzizaRohoni

ADS