KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Ninaye Rafiki Naye

 1. Ninaye Rafiki Naye
  Alinipenda mbele;
  Kwa kamba za pendo zake
  Nimefungwa milele;
  Aukaza moyo wangu,
  Uache mageule,
  Mimi wake, Yeye wangu
  Ndimi naye milele.

 2. Ninaye Rafiki Naye
  Aliyenifilia;
  Alimwaga damu yake
  Kwa watu wote pia;
  Sina kitu mim pia;
  Nikiwa navyo tele;
  Pia vyote ni amana
  Ndimi wake milele.

 3. Ninaye Rafiki Naye
  Uwezo amepewa;
  Atanilinda mwenyewe,
  Juu tachukuliwa;
  Nikitazama Mbinguni
  Hupata nguvu tele;
  Sasa natumika chini.
  Kisha juu milele.

 4. Ninaye Rafiki Naye
  Anao moyo mwema;
  Ni Mwalimu, Kiongozi,
  Mlinzi wa daima;
  Ni nani wa kunitenga
  Na Mpenzi wa mbele?
  Kwake nimetia nanga,
  Ndimi wake milele.


TenzizaRohoni

ADS