KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Nina Haja Nawe

 1. Nina haja nawe
  Kila saa:
  Hawezi mwingine
  Kunifaa.

 2. Yesu, nakuhitaji
  Vivyo kila saa!
  Niwezeshe, Mwokozi,
  Nakujia.

 3. Nina haja nawe;
  Kaa nami,
  Na maonjo haya,
  Hayaumi.

 4. Nina haja nawe;
  Kila hali,
  Maisha ni bure,
  Uli mbali.

 5. Nina haja nawe;
  Nifundishe
  Na ahadi zako
  Zifikishe.

 6. Nina haja nawe;
  Mweza yote,
  Ni wako kabisa
  Siku zote.


TenzizaRohoni

ADS