KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Nilikuwa Kondoo Aliyepotea
I was a wandering sheep

 1. Nilikuwa kondoo aliyepotea,
  Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
  Nilikuwa mwana asiyesikia,
  Sikupenda Baba yangu wala kutulia.

 2. Na Mchunga Mweme alinitafuta,
  Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
  Karibu ya kufa kwa kiu na kwa njaa,
  Waliniona mnyonge, waliniokoa.

 3. Yesu ni Mchunga, mwenziwe hapana,
  Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana;
  Kwa vidonda vyangu alitia dawa,
  Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.

 4. Nilikuwa kondoo aliyepotea,
  Sasa nampenda Baba, na Mchunga pia;
  Kwanza nilitanga na kukosa sana,
  Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.


TenzizaRohoni

ADS