KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Ni Wako Wewe
(I am Thine, O Lord. I have heard Thy voice)

 1. Ni wako Wewe, nimekujua,
  Na umeniambia;
  Lakini Bwana, nataka kwako,
  Nizidi kusongea.

 2. Bwana vuta, vuta, nije
  Nisongee,
  Sana, kwako Mtini,
  Bwana vuta, vuta nije
  Nisongee,
  Pa damu ya thamani.

 3. Niweke sasa nikatumike
  Kwa nguvu za neema;
  Uyapendayo nami nipende,
  Nizidi kukwandama.

 4. Nina furaha tele kila saa
  Nizungumzayo kwako,
  Nikuombapo nami napata
  Kujua nia yako.

 5. Mapenzi yako hayapimiki,
  Ila ng'ambo ya liko,
  Anasa pia sitazijua
  Bila kufika kwako.


TenzizaRohoni

ADS