KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Ni Tabibu wa Karibu

 1. Ni tabibu wa karibu;
  Tabibu wa ajabu;
  Na rehema za daima;
  Ni dawa yake njema.

 2. Imbeni, malaika.
  sifa za Yesu Bwana;
  Pweke limetukuka
  Jina lake Yesu.

 3. Hatufai kuwa hai,
  Wala hatutumai,
  Ila yeye kweli ndiye,
  Atupumzishaye.

 4. Dhambi pia na hatia
  Ametuchukulia;
  Twenendeni na amani
  Hata kwake mbinguni.

 5. Huliona tamu jina,
  La Yesu kristo Bwana,
  Yuna sifa mwenye kufa
  Asishindwe na kufa.

 6. Kila mume asimame,
  Sifa zake zivume;
  Wanawake na washike,
  Kusifu jina lake.

 7. Na vijana wote tena,
  Wampendao sana,
  Waje kwake wawe wake
  Kwa utumishi wake.


TenzizaRohoni

ADS