KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Ni Siku Kuu Siku Ile

 1. Ni siku kuu siku ile,
  Ya kumkiri Mwokozi!
  Moyo umejaa tele,
  Kunyamaza hauwezi.

 2. Siku kuu! Siku kuu!
  Ya kuoshwa dambi
  Zangu kuu!
  Hukesha na kuomba tu,
  Ananiongoza miguu.
  Siku kuu! siku kuu!
  Ya kuoshwa dhambi
  Zangu kuu.

 3. Tumekwisha kupatana
  Mimi wake, yeye wangu,
  Na sasa nitamwandama,
  Nikiri neno la Mungu.

 4. Moyo tulia kwa Bwana,
  Kiini cha raha yako,
  Huna njia mbili tena;
  Yesu ndiye njia yako.

 5. Nadhiri yangu ya mbele,
  Nitaiweka daima,
  hata ije siku ile,
  ya kwonana kwa salama.


TenzizaRohoni

ADS