KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Ni Salama Rohoni Mwangu
When peace like a river

 1. Nionapo amani kama shwari,
  Ama nionapo shida,
  Kwa mambo yote umenijulisha
  Ni salama rohoni mwangu.

 2. Salama rohoni,
  Ni salama rohoni mwangu.

 3. Ingawa Shetani atanitesa,
  Nitajipa moyo kwani
  Kristo ameona unyonge wangu,
  Amekufa kwa roho yangu.

 4. Dhambi zangu zote, wala si nusu,
  Zimewekwa Msalabani.
  Wala sichukui Iaana yake,
  Ni salama rohoni mwangu.

 5. Ee Bwana himiza siku ya kuja,
  Panda itakapolia;
  Utakaposhuka sitaogopa
  Ni salama rohoni mwangu.


TenzizaRohoni

ADS