KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Naweka Dhambi Zangu
(I lay my sins on Jesus)

 1. Naweka dhambi zangu
  Juu yake Bwana
  Kuziondoa, kwangu
  Hulemea sana;
  Na uaili wangu
  Ameuondoa;
  Dawa yangu ni damu,
  Kwa hiyo napoa.

 2. Na uhitaji wangu
  Nitamjuvisha,
  Kwa upungufu wangu
  Yeye anatosha
  Majonzi yangu yote
  Na mizigo yangu,
  Atachukua vyote
  Yesu Bwana wangu.

 3. Na roho yangu nayo
  Imechoka sana;
  Namletea hiyo
  Ilindwe na Bwana;
  Ni jema jina lake,
  Nalo lapendeza,
  Imanweli na kwake
  Tutalitukuza.

 4. Natamani daima
  Niwe kama Bwana.
  Mpole, tena mwema,
  Wa mapenzi sana;
  Zaidi natamani
  Kwenda kwake juu
  Nikaone mbinguni
  Enzi yake kuu.


TenzizaRohoni

ADS