KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Nataka Nimjue
(Yesu More about Jesus)

 1. Nataka nimjue Yesu,
  Na nizidi kumfahamu,
  Nijue pendo lake, na
  Wokovu wake kamili.

 2. Zaidi, zaidi, nimfahamu
  Yesu, Nijue pendo lake, na
  Wokovu wake kamili.

 3. Nataka nione Yesu.
  Na nizidi kusikia
  Anenapo Kitabuni,
  Kujidhihirisha kwangu.

 4. Nataka nifahamu, na
  Nizidi kupambanua
  Mapenzi yake, nifanye
  Yale yanayompendeza.

 5. Nataka nikae naye,
  Kwa mazungumzo zaidi,
  Nizidi kuwaonyesha,
  Wengine wokovu wake.


TenzizaRohoni

ADS