KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Namwandama Bwana
(When we walk with the Lord)

 1. Namwandama Bwana kwa alilonena,
  Njia yangu huning'azia;
  Nikimridhisha atanidumisha
  Taamini nitii pia.

 2. Amini utii, njia pweke ni hii
  Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.

 3. Giza sina kwangu wala hata wingu,
  Yeye mara huviondoa;
  Woga, wasiwasi, sononeko, basi,
  Huamini nitii pia.

 4. Masumbuko yote, sikitiko lote:
  Kwa mapenzi hunilipia;
  Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki,
  Taamini nitii pia.

 5. Mimi sitajua raha sawasawa,
  IIa yote Yesu kumpa;
  Napata fadhili na radhi kamili,
  Taamini nitii pia.

 6. Nitamfurahia na kumtumaini,
  Majumbani na njia-njia;
  Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
  Huamini nitii pia.


TenzizaRohoni

ADS