KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Mwokozi Umeokoa

 1. Mwokozi umeokoa,
  Nimekuwa wako Wewe.
  Damu imenisafisha,
  Sifa kwa Mwana Kondoo.

 2. Utukufu, Aleluya!
  Sifa kwa Mwana Kondoo!
  Damu imenisafisha,
  Utukufu kwa Yesu!

 3. Nilijitahidi sana
  Ila sikupata raha;
  Bali kwa kumtegemea
  Nilipata baraka.

 4. Daima namwegemea,
  Damu ikifanya kazi,
  Nikioga kwa chemchemi
  ltokayo Mwokozi.

 5. Sasa nimewekwa wakfu:
  Nitaishi kwako Wewe;
  Fahari nashuhudia
  Ya wokovu wa bure.

 6. Nasimama kwake Yesu,
  Ameponya roho yangu:
  Ameniondoa dhambi.
  Anifanye mzima.

 7. Nilikuwa kifungoni,
  Niliteswa na dhambi.
  Nilifungwa minyororo.
  Yesu akanifungua.

 8. Sifa, ameninunua!
  Sifa, nguvu za wokovu!
  Sifa, Bwana huhifadhi!
  Sifa zake milele.


TenzizaRohoni

ADS