KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Mwokozi Moyoni Mwangu
Since Jesus came into my heart

 1. Tangu siku hiyo aliponijia,
  Akae moyoni mwangu,
  Sina giza tena, ila mwanga pia
  Kwa Yesu Mwokozi wangu.

 2. Amani moyoni mwangu,
  Kwa Yesu, Mwokozi wangu,
  Sina shaka kamwe,
  Kwa sababu Yeye
  Yu nami moyoni mwangu.

 3. Sina haja tena ya kutanga-tanga,
  Ndiye Kiongozi wangu.
  Dhambi zangu zote zimeondolewa,
  Na Yesu, Mwanawe Mungu.

 4. Matumaini yangu ni ya hakika,
  Katika Mwokozi wangu.
  Hofu zangu na hamu zimeondoka.
  Kwa kuwa ninaye Yesu.

 5. Siogopi tena nikiitwa kufa,
  Yu nami daima, Yesu.
  Mlango wa Mbinguni ni Yeye pia,
  "Talipa humo kwa damu."

 6. Nitaketi na yeye huko milele,
  Nisifu Mwokozi wangu.
  Nina raha moyoni majira yote
  Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.


TenzizaRohoni

ADS