KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Mwenye Dhambi Huna Raha
(Come, ye sinners, poor and wretched)

 1. Mwenye dhambi huna raha.
  Sikiza nakusihi,
  Utapata msamaha
  Kwake Yesu Mwokozi!
  Njoo hima, njoo hima,
  Naye atafurahi.

 2. Yesu anakwita sana
  Naye yuko Mbinguni:
  Hofu ya kifo hapana
  Kwake ukiamini.
  Njoo hima, njoo hima,
  Utapata amani.

 3. Hatakwita siku zote;
  Ni ya sasa nafasi.
  Lete na uchafu wote,
  Kukawa haipasi.
  Njoo hima, njoo hima,
  Ni wokovu halisi.

 4. Uzima uko kwa Bwana
  Twae uzima hasa!
  Bure utapatikana,
  Wokovu twae sasa!
  Njoo hima, njoo hima,
  Twae utakatifu.


TenzizaRohoni

ADS