KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Mungu Mtukufu Aliye Bwana

 1. Mungu mtukufu aliye Bwana,
  Akamtoa Yesu mwana mpendwa;
  Akawa dhabihu kwa dhambi zote,
  Kufungua njia kwa watu wote.

 2. Msifuni, msifuni Nchi imsikie,
  Msifuni, msifuni, Bwana mshangilie;
  Njoni kwake Baba, kwa Yesu Mwana,
  Mpeni heshima, aliye Bwana.

 3. Ukombozi wetu, tendo la Mungu,
  Ni ukamilifu kwa kila mtu;
  Mwenye ukosefu akimwamini,
  Atasamehewa na Yesu, kweli.

 4. Ametufundisha mambo ya mbingu,
  Tukafurahishwa na Mwana Mungu;
  Ametuinua tukae naye,
  Atatuongoza hata milele.


TenzizaRohoni

ADS