KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Mtazame Huyo! Aliyeangikwa Juu
(There is life for a look at the Crucified One)

 1. Mtazame huyo! Aliyeangikwa juu
  Hivi sasa upate ishi.
  Mwenye-dhambi dhaifu, mtazame tu
  Wala usifanye tashwishi.

 2. Tazama! Tazama! Tazama uishi!
  Mtazame huyo aliyeangikwa juu
  Hivi sasa upate ishi.

 3. Kama Mwana Kondoo hakuondoa dhambi,
  Na makosa yako maovu!
  Kama deni zetu zote hakulipa
  Mbona imemwagika damu?

 4. Si kutubu na sala ikomboayo
  Ila damu ndiyo salama;
  Na allyeimwaga aweza, sasa,
  Dhambi zako kukufutia.

 5. Usiwe na shaka, Mungu amesema.
  Hakuna alilolisaza;
  Hapo alipokuja alitimiza
  Kazi zote alizoanza.

 6. Basi twae uzima kwa kufurahi
  Upokee kwa Bwana, sasa;
  Ujijue hakika kwake kuishi
  Yesu aishiye kabisa.


TenzizaRohoni

ADS