KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Kazi Yangu Ikiisha

 1. Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
  na kuvaa kutokuharibika,
  nitamjua Mwokozi nifikapo ng'amboni;
  atakuwa wa kwanza kunilaki.

 2. Nitamjua, nitamjua,
  nikimwona uso kwa uso;
  Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

 3. Furaha nitapata nikiona makao,
  Bwana aliyotuandalia;
  nitamsifu mwokozi, kwa rehema na pendo,
  vilivyonipa pahali Mbinguni.

 4. Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
  nitawaona tena huko juu;
  lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
  nataka kumwona Mwokozi kwanza.

 5. Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
  pasipo machozi wala huzuni.
  Nitauimba wimbo wa milele;
  lakini nataka kumwona Mwokozi kwanza.


TenzizaRohoni

ADS