KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Kale Nilitembea

 1. Kale nilitembea,
  Nikilemewa dhambi
  Nilikosa Msaada,
  Kuniponya mateso.

 2. Usifiwe Msalaba!
  Lisifiwe kaburi!
  Linalozidi yote,
  Asifiwe Mwokozi!

 3. Hata nilipofika,
  Mahali pa Msalaba,
  Palinifaa sana,
  Sitasahau kamwe.

 4. Hicho ndicho chanzo
  Cha kufurahi kwangu.
  Hapo ndipo mzigo,
  Uliponituliwa.

 5. Panapo Msalaba,
  Kinatolewa cheti
  Cha kuingia Mbinguni,
  Kisicho cha kanisa.

 6. Yule bwana mjinga,
  Likwenda bila cheti,
  Kitumai kwingia,
  Kana walio nacho.

 7. Lipofika langoni,
  Akaulizwa cheti
  Cha kumwonyesha
  Bwana Akakutwa hanacho.

 8. Lituhuzunishalo,
  Ni ninyi msio nacho,
  Kuwa kama mjinga,
  Kwa siku ya arusi!

 9. Ubavuni mwa Yesu,
  Mlitokea damu,
  Chemchemi ya uzima,
  itakasayo roho.

 10. Jitahidi wingie,
  Damuni mwa Mwokozi,
  Utafutiwa dhambi,
  Toka rohoni mwako.


TenzizaRohoni

ADS