KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Jina la Yesu, Salamu!

 1. Jina la Yesu, salamu!
  Lisujudieni,
  Ninyi Mbinguni, hukumu
  Na enzi mpeni.

 2. Enzi na apewe kwenu,
  Watatea dini;
  Mkuzeni Bwana wenu,
  Na enzi mpeni.

 3. Enyi mbegu ya rehema,
  Nanyi msifuni;
  Mmeponywa kwa neema,
  Na enzi mpeni.

 4. Wenye dhambi kumbukeni,
  Ya Msalabani,
  Kwa furaha msifuni,
  Na enzi mpeni.

 5. Kila mtu duniani
  Msujudieni,
  Kotekote msifuni,
  Na enzi mpeni.

 6. Sisi na wao pamoja
  Tu mumo sifani,
  Milele sifa ni moja,
  Ni "Enzi mpeni."


TenzizaRohoni

ADS