KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Deni Ya Dhambi Ilimalizika

 1. Deni yangu ya dhambi,
  Yesu amelipa,
  Kwake Msalabani
  Nilipewa uzima.

 2. Deni ya dhambi, Msalabani,
  Ilimalizikia, Ni huru kabisa.

 3. Bwana Yesu asema,
  "Mwanangu dhaifu",
  Uwezo na ushindi,
  Hupatikana kwangu.

 4. Bwana, kweli naona,
  Nguvu zako pekee
  Huondoa ukoma,
  Niwe kipya kiumbe.

 5. Sina wema moyoni,
  Nidai neema,
  Nakubali kabisa,
  Kwa damu kusafiwa.

 6. Hata huko Mbinguni,
  Miguuni pake,
  "Yesu alinifia,"
  Nitaimba milele.


TenzizaRohoni

ADS