KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Cha Kutamaini Sina

 1. Cha kutamaini sina,
  Ila damu yake Bwana,
  Sina wema wa kutosha,
  Dhambi zangu kuziosha;

 2. Kwake Yesu nasimama,
  Ndiye mwamba ni salama,
  Ndiye mwamba ni salama.

 3. Njia yangu iwe ndefu,
  Yeye hunipa wokovu;
  Mawimbi yakinipiga,
  Nguvu zake ndiyo nanga.

 4. Damu yake na sadaka,
  Nategemea daima,
  Yote chini yakiisha,
  Mwokozi atanitosha.

 5. Nikiitwa hukumuni,
  Rohoni nina amani;
  Nikivikwa haki yake,
  Sina hofu mbele zake.


TenzizaRohoni

ADS