KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Bwana U Sehemu Yangu

 1. Bwana u sehemu yangu,
  Rafiki yangu, wewe,
  Katika safari yangu,
  Tatembea na wewe.

 2. Pamoja na wewe,
  Pamoja na wewe,
  Katika safari yangu,
  Tatembea na wewe.

 3. Mali hapa sikutaka,
  Ili niheshimiwe,
  Na yanikute mashaka,
  Sawasawa na wewe.

 4. Niongoze safarini,
  Mbele unichukue,
  Mlangoni mwa mbinguni,
  Niingie na wewe.


TenzizaRohoni

ADS