KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Baba Yetu Aliye Mbinguni
I am so glad that our Father in heaven

 1. Baba Yetu aliye Mbinguni
  Amenifurahisha yakini
  Kuniambia mwake Chuoni
  Ya kuwa nami Yesu pendoni.

 2. Anipenda Mwokozi Yesu,
  Anipenda, anipenda;
  Anipenda Mwokozi Yesu,
  Anipenda mimi.

 3. Nimuachapo kutanga mbali
  Yeye yu vivyo, hupenda kweli.
  Hunirejeza kwake moyoni;
  Kweli yu nami Yesu pendoni.

 4. Anipenda! Nami nampenda;
  Kwa wokovu alionitenda;
  Akanifia Msalabani
  Kwa kuwa nami Yesu pendoni.

 5. Haya kujua yanipa raha;
  Kumuamini kuna furaha;
  Humfukuza mara Shetani,
  Kwona yu nami Yesu pendoni.

 6. Sifa ni nyingi asifiwazo,
  Moja ni sana katika hizo,
  Wala siachi, hata Mbinguni,
  Kwimba, "Yu nami Yesu pendoni.


TenzizaRohoni

ADS