KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Anisikiaye Aliye Yote
(Whosoever will)

 1. Anisikiaye, aliye yote;
  Sana iitangae, wajue wote,
  Duniani kote neno wapate,
  Atakaye na aje!

 2. Ni "Atakaye," ni "Atakaye,
  Pwani hata bara, na litangae:
  Ni Baba Mpenzi alinganaye
  Atakaye na aje.

 3. Anijiliaye, Yesu asema,
  Asikawe, aje hima mapema;
  Ndimi Njia, Kweli, ndimi Uzima;
  Atakaye na aje!

 4. Atakaye aje, ndiyo ahadi,
  Atakaye hiyo, haitarudi!
  Atakaye lake, ni la abadi!
  Atakaye na aje.


TenzizaRohoni

ADS