KASISI w3Cert.
TenzizaRohoni

ADS

TENZI ZA ROHONI

Akifa Yesu Nikafa Naye

 1. Akifa Yesu nikafa naye,
  Uzima upya huishi naye;
  Humtazama mpaka aje;
  Nyakati zote ni wake Yeye.

 2. Nyakati zote nimo pendoni,
  Nyakati zote ni uzimani,
  Humtazama hata atokee,
  Nyakati zote mimi ni wake.

 3. Vita sipigi visivyo haki,
  Na Bwana wangu hapiganiki;
  Beramu yake haitwaliki,
  Napo po pote hila sitaki.

 4. Sina mashaka, akawa mbali;
  Mizigo yote aihimili;
  Ananituliza Imanweli,
  Nyakati zote mimi husali.

 5. Sina huzuni na mimi sidhii;
  Simwagi chozi, wala siguni;
  Sikuti afa, ila Kitini
  Daima hunifikiri mimi.

 6. Kila unyonge huusikia;
  Kila ugonjwa kwake hupoa
  Yesu ni mwenye kuniokoa
  Nyakati zote hunijalia.


TenzizaRohoni

ADS